Huduma Zetu

Huduma Za USCF TAKWIMU

USCF-CCT TAKWIMU huendesha shughuli mbalimbali za kiroho na kijamii:

  • Ibada za Kila Wiki
  • Masomo ya Biblia
  • Maombi na Kuliombea Taifa
  • Mafundisho na Semina
  • Huduma za Kijamii
  • Uinjilisti

"We serve the living God."

Mahali ambapo wanafunzi wanakua kiroho na kujifunza kuishi maisha yenye maana ndani ya Kristo.

Uinjilisti & Umisheni

Umisionari ni kitendo cha kueneza dini Fulani (kikristo) kwa wasio waumini wa dini hiyo.

Tunafurahia kutangaza mission zetu, ambazo huanza kwa maandalizi mazito ili kupata ruhusa na maeneo yanayohitajika.

Budekwa Mission

New beginning in Christ

Nanyamba Mission

Till the whole world knows

Nanyamba Mission

Till the whole world knows

Kabla ya mission, tunashiriki katika maombi ili kujiandaa kiroho. Tunafanya shughuli za visitation na semina mbalimbali.

Wakati wa mission, lengo letu kuu ni kufanya mikutano ili kushiriki ujumbe wa matumaini na wokovu.

Tunashiriki katika shughuli za kijamii na bonanza fupi siku ya mwisho.

Kambi Ya Maombi

Kambi yetu ya Maombi hufanyika ili kutuandaa kiroho na kukuza ukuaji wa imani kupitia mafundisho na shughuli.

  • Kuombea semester yenye mafanikio
  • Mafundisho ya kidini
  • Michezo ya afya ya mwili na kiroho
  • Maombi ya kina

Kabla ya kambi, tunashiriki katika maombi ya awali. Wakati wa kambi, kuna vipindi vya maombi ya kipekee na kufunga.

Pia kuna maombi maalumu ya kuombea taifa na jamii.

Mahafali

Kama USCF, tunafanya mahafali kwa njia ya kipekee kwa ajili ya kuwaenzi wahitimu:

Ibada ya Shukrani & Shuhuda kwa wahitimu
Hotuba za Kuhamasisha
Utoaji wa Zawadi & Vyeti

Lengo letu ni kuhakikisha wahitimu wanahisi kuthaminiwa na wanajengewa msingi imara wa maisha baada ya chuo.

Matendo Ya Huruma

USCF inajitolea kuleta mabadiliko chanya kwa jamii kupitia juhudi zetu za hisani.

Msaada wa chakula na mavazi

Msaada wa elimu

Utembeleaji wa vituo vya watoto yatima

Tunatekeleza maadili ya Kikristo ya upendo, huruma, na ukarimu.

Semina

USCF inajitahidi kukuza ukuaji wa kiroho, kiakili, na kibinafsi kwa wanafunzi.

Semina ya Umisheni

Inayojikita katika utume na huduma

Semina za Maisha ya Kikristo

Masuala ya ukuaji wa kiroho na uongozi

Zinakusudiwa kuwahamasisha, kuwawezesha, na kuwajengea uwezo wanafunzi.

USCF CCT TAKWIMU SHOP

Duka letu linatoa bidhaa mbalimbali zinazokidhi mahitaji yako.

Nunua Sasa

Furahia bidhaa zetu za kipekee!

Contact Us

Phone: +255 755 327 135

Email: uscftakwimu@gmail.com

Address: EASTC, Dar es Salaam, Tanzania

Connect With Us


Copyright © 2025 USCF CCT TAKWIMU. All Rights Reserved.. Designed and developed by USCF IT Department.